Kama unakumbuka miezi 3 iliyopita Shilole alienda kufanya show nchini Ubelgiji wakati akitumbuiza jukwaani kwa bahati mbaya sehemu ya kifua chake(TITI) ilijitokeza kwa nje baadae picha zikapigwa na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya hukumu hiyo millardayo.com ilipata nafasi ya kuongea na Shilole ambapo aliuliza maswali manne kwa Basata kama wasimamizi wa shughuli zote zinazohusu sanaa kwa Tanzania.
1.Kwanini barua imekuja baada ya kupost show yangu ya kwenda Marekani kufanya show?
2.Mmenifungia muziki wangu,Mnataka nikaishi wapi?na mnasema vijana tujiajiri,ajira niliyojiajiri ni hii mnataka nifanye ipi?
3.Nina familia ya watu 10 ndani kwangu,wote wananitegemea wengine wanasoma Boarding,nina watoto yatima wengine wanasoma kupitia muziki huu huu na ninalipa kodi ya nyumba,Mnataka Basata tufanye nini?
4.Ninahangaika,ninapambana na kazi zangu kwa nguvu zangu,Mnataka nikajiuze nipate ukimwi?mnataka nikabebe Dawa za kulevya nikauwawe?kwa sababu najituma kwa kazi yangu na nguvu yangu kama mnavyoona kwenye jukwaa hata vitabu vya Mungu vinasema asiyefanya kazi na asile