Akizungumza na gazeti la Filamu, Amanda alisema kwa mwezi huu hatoonekana akikatiza mitaani na nguo zilizobana kiasi cha kuonyesha maungo yake ya sehemu za siri bali atakuwa anajisitili ili kujiepusha na kitendo cha kuwaingiza majaribuni wanaume hasa walio kwenye mfungo na mpaka mwezi huu unaisha atakuwa amezoea kuvaa nguo hizo.
“Naweza kusenma kuwa mfungo wa mwezio Ramadhani umeniweka kando na skendo hasa za kuvaa nguo fupi ambazo huwa zinawaingiza kwenye mitego wanaume wasio weza kujizuia wanapoona maungo ya wanawake hasa waliovaa nguo zenye ushawishi,” alisema Amanda.
Aidha, Amamnda aliwataka hata wasanii wenzake hasa wa kike kuheshimu kipindi hiki kwani ni cha kuvuna neema kutoka kwa Mungu kutokana na kutibu madhambi yote yaliyofanyika siku za nyuma na ikiwezekana na wao uwe mwanzo wa kubadilishwa huhusu kuachana na skendo za kujitakia hasa zile za kutengeneza ili waendelee kusomeka kwenye magazeti.
Tanuru la Filamu