Akizungumza na Leo Tena ya Clouds Fm,alisema kuwa wao ni vioo vya jamii na wanapendwa na watu wengi na anapoona yanatokea mambo hayo kwenye mitandao hiyo ya kijamii hawezi kufanya chochote na kuwaingilia mashabiki hao.
‘’Kiukweli sifurahishwi na timu hizi na naona kinachoendelea kwenye mitandao lakini siwezi kufanya chochote na kuwaingilia mashabiki,ila ushauri wangu ni bora wangeacha tu,’alisema Kiba.