Rose Ndauka alikubali kwamba aliyestahili ni Irene Paul kwa kuwa ni changamoto kwake na kwa wasanii wengine.
“Nakubaliana na matokeo sisikitiki kukosa tuzo hiyo, siwezi kuwalalamikia wananchi kwani wao ndio walioona filamu zilizoshindanishwa wakachagua,’’ alisema Rose na kuongeza:
“Kwenye tuzo nyingine mbona huwaga nashinda nao hawachukii kushinda kwangu, hivyo nami sipaswi kuchukia nakubaliana na matokeo nitafanya kazi nzuri zaidi ili nichukue tuzo hiyo mwakani,” alimaliza Rose.
Mtanzania