Kitendo cha Wema ambaye alikuwa ni mpezi wa Diamond kumsapoti Ali Kiba ambaye kwasasa inaonekana ndiye msanii mwenye ushindani (Kisanaa) na Diamond kimechukuliwa kwa mitazamo tofauti na mashabiki wa mastaa hawa.
Team za mastaa hawa mtandaoni maarufu kama Team Mond, Team Kiba na Team Wema wamekua na mitazomo tofauti juu ya hiki anachokifanya Wema na hadi kufikia kutoleana lugha chafu wakati team Diamond wanaponda; huku team Kiba na Wema kuwa upande mmoja.
“Unapenda kiba wakati umetemwa na chibu alafu hukumbuki arusha umefukuzwa kwa show ya kiba aibu huna kweli we mdada team platnamz hapa”-mmoja alikomenti
Team Wema na Team Kiba wanamuunga mkono
“Halafu watu wengine viazi sana humu ndani kapostiwa King king king kiba mara ooooh chibu who is the Chibu by the way haaaaaaaaa. Acheni usechu kma ni diamond huko huko kwenu uhanithihatutaki siye halaaaaa hata kama ajibebisha mwataka ajibebishe kwenu khaaaaa. Hebu legooooooo Wematwende sawa. Vote for King baaaaanaaaa Ama niniiiiiiiii”-mmoja alikomenti
Wema Sepetu akiwa ndiye staa wa bongo mwenye followers wengi zaidi kwenye mtandao picha wa instagram (587,000 hadi sasa) amekuwa akiweka ‘posters’ za Ali Kiba na kuandika maneno ya kumsifia kama;
“Im thinking Eye candy.... Dats da right post...”
“Too much cuteness on this poster tho......”
“Im thinking Eye candy.... Dats da right post...”
“Campaign Inaendelea ama nene.... Such a cutie...!!! Like I said, either he gets it or nat, He still Fiiiiiiiiiiiiine....! Hihihihihi.... JustSayin...!!!”
NB: Mara kadhaa Wema kwenye mahojiano amekua akisema wazi kuwa yeye ni mshabiki wa Diamond.