Linex kwenye Interview na sammisago.com anasema wimbo wake wa Wema Kwa Ubaya video imeshalipiwa na Mhe Zitto Kabwe kwa Adam Juma na kwamba muda wowote itatoka.
Kuhusu kazi aliyofanya na Diamond, Linex ameweka wazi kuwa ni kazi itakayolenga level za kimataifa zaidi.
“Ni muda wa kufanya mambo makubwa zaidi kwenye muziki na imani yangu ni kuwa kazi hii niliyofanya na Diamond ‘Salima’ itafanya vizuri kama itakuwa na video bora na usimamizi mzuri nje na ndani ya Bongo”
Linex ni miongoni mwa wasanii wanaojituma sana Tanzania na utakumbuka kuwa aliwahi kumlipa zaidi ya Milioni moja Video Queen Jackie Cliff ilikuigiza kwenye video yake ya Kimugina.