Saturday, June 21, 2014

Manji avunja ukimya, azungumzumzia tuhuma za kung'ang'ania madaraka Yanga

0
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuph Mehboob Manji amevunja ukimya na kuzungumzia madai ya baadhi ya wanachama wa Yanga kuwa anang’ang’ania madaraka na kwamba muda wake wa kuingoza timu hiyo umekwisha.
Yusuph Manji amekanusha uwepo wa wanachama 250 wanaopinga maazimio ya mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika June 01 mwaka huu ambao ulimpa ridhaa mwenyekiti huyo kuendelea kukaa madarakani kwa mwaka mmoja zaidi.
Amesema si kweli kwamba yeye ana uchu wa madaraka na kama kuna mwanachama yoyote anaepinga maazimio hayo anaruhusiwa kwenda makao makuu ya klabu hiyo ajiorodheshe ili demokrasia ifuatwe.
Ameongeza kuwa sera yake sio kumsababisha mtu afukuzwe uanachama bali ni kuzidi kuongeza wanachama.

FROM
http://timesfm.co.tz

Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment