Iliwahi kutokea Tabata Dar es salaam akakamatwa askari feki wa
usalama barabarani ambae ni mzee aelikua anavalia sare na madereva
walikua wanajua kweli huyu ni askari na faini na rushwa akawa anazilamba
kama kawaida.
Stori nyingine kwenye headlines sasa hivi ni za Mwanajeshi feki
nchini Kenya ambapo kituo cha TV cha K24 ndio kimeripoti hii stori kwa
kusema jamaa alishtukiwa na Mwanajeshi halisi wa nchi hiyo.Huyu jamaa mwenye umri wa miaka 23 alikamatwa wakati akiwa anasafiri,
anaitwa Robert Mutuku na anakiri alipata hizi jezi za jeshi kutoka kwa
rafiki yake ambae alikua anamtafutia kibarua jeshini.
Akiwa tayari anashikiliwa na polisi, Mutuku ambae pia alikua na
kitambulisho feki cha jeshi amekaririwa akisema ‘ni kazi nilikua naitaka
ndio maana niliomba hizi nguo kwa sababu naipenda hii kazi’