Wataalamu wa Mambo wanaamini kuwa Female Mc Witnesz kwa wakati huu ana ujauzito wa msanii mwenzake Ochu Sheggy, hisia hizo zimekuja baada ya Witnesz kupost kwenye Facebook picha hiyo hapo juu ikimwonyesha akiwa ameshikwa tumbo na Ochu tumbo linaonekana limevimba mithili ya mjamzito na Witnesz akaandika juu yake "Ni kweli lakini hayakuhusu!" mwisho wa kunukuu, kama ni kweli anaujauzito safi sanaaa kwani wawili hao wana zaidi ya mwaka mmoja wakiwa katika mahusiano Nginga hadi wakaamua kuishi pamoja maeneo ya Kijitonyama Akachube Road.
Hii si mara ya kwanza kwa Witnesz kupata ujauzito, mwaka 2012 aliwahi kupata Ujauzito wa aliyekua mume wake (Mokeyz) lakini kwa bahati mbaya mtoto hakua rizki.
Taarifa za Ujauzito wa Witnesz bado hazijawa Rasmi, naendelea kumtafuta ili atuthibitishie.