Rapper Trina amefunguka leo kwenye interview tofauti alizofanyiwa kuhusu mahusiano yake na Rapper wa Bad Boys Entertainment French Montana. Hivi karibuni wameonekana maeneo tofauti ya starehe na kazi huku wakiwa karibu sana [Zero Distance] kitu kilichofanya wafatiliaji wa mambo kuuliza je ni wapenzi au wana mahusiano zaidi ya ufariki.
Trina amesema" French Montana ni kijana mzuri sana mwenye tabia na heshima ya kuigwa, mahusiano yao ni ya kirafiki tu na sio mapenzi, wamekuwa wakifanya kazi pamoja toka walivyo kutana na Trina amejifunza mengi kutoka kwa French. Montana amesikiliza kazi zangu mpya na amenipa ushauri kuhusu kubadilika na maendeleo ya mziki wangu alimaliza Trina.
Hii story inatukumbusha wakati mapenzi ya Ciara na Future yanaaza, Walikuwa kama Trina na Montana