Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro na kusomewa mashitaka matatu yanayomkabili.
Ponda alifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la Polisi waliokuwa na mbwa baada ya kupokelewa kutoka katika Viwanja vya Gymkhana alipotua kwa helkopta majira ya saa tatu asubuhi akitolewa katika Gereza la Segerea, jijini Dar es Salaam.
Makosa matatu aliyosomewa Sheikh Ponda na wakili wa serikali, Bwana Bernard Kongola mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro Richard Kabate ni pamoja na Kutotii amri ya mahakama, uchochezi na kutaka kuvuruga amani ambayo mtuhumiwa ameyakana.
Mawakili wa upande wa mtuhumiwa walikuwa Ignas Pungu na Bantalomeo Tarimo, wakati upande wa serikali kulikuwa na Benedict Kongola, Gloria Rwakibalila na Asnab Mhando.
Kesi hiyo itasikilizwa tena Agosti 28 mwaka huu na mtuhumiwa amerudishwa Segerea jijini Dar es Salaam kwa usafiri uleule wa helkopta.
via http://www.globalpublishers.info/
via http://www.globalpublishers.info/