Wednesday, July 24, 2013

Mr Nice Ajitutumua Apanga Mashambulizi, Na Hivi Ndivyo 'Atakavyoilipua' Grandpa Records Kesho

0
Baada ya taarifa za hapa na pale kuhusiana na msanii Mr. Nice kuhaha na mambo yake kuyumba huko Kenya hasa baada ya kupigwa chini na lebo ya Grandpa, Sasa habari mpya ni kwamba, msanii huyu amepata shavu jingine na anatarajia kusaini mkataba mpya na lebo mpya inayotambulika kama Candy N Candy ya huko huko Nairobi.         
              
Cha kusisimua zaidi juu ya hili, ni taarifa kwamba Mr Nice atasaini mkataba huo mpya siku ya kesho [25th July, 11:00am] ambapo pia na yeye kwa upande wake ataweka wazi taarifa za upande wa pili kuhusiana na 'Mabaya' ya Grandpa Records ambayo yamesababisha yeye kushindwa kufanya kazi na lebo hiyo.

Itakumbukwa kuwa Grandpa kama lebo wao kwa upande wao walikwishatoa sababu za kushindwa kufanya kazi na Mr Nice, miongoni mwa sababu hizi ukiwepo uvivu na ulevi, hivyo sasa mitaa yote imekaa macho juu kusikilizia Mr Nice na yeye akifunguka kwa upande wake juu ya Grandpa Records.
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment