Tuesday, July 16, 2013

Meya CCM akalia kuti kavu Arusha

0

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (katikati) akizungumza kwenye Ofisi za Halmashauri ya Arusha akiwa na madiwani wapya wa Chadema waliochaguliwa juzi. Kutoka kushoto mstari wa mbele ni Jeremiah Mpinga (Elerai), Edmund  Kinabo (Themi), Kessy Lewi (Kaloleni) na Rayson Ngowi (Kimandolu). 
Arusha. Kitendo cha Chadema kutetea viti vyake vinne vya udiwani kwenye uchaguzi mdogo wa juzi, kimetafsiriwa kwamba ni kumfanya Meya wa Jiji la Arusha, Gaudence Lyimo kukalia kuti kavu. Kwa ushindi wake huo, Chadema kimefikisha viti 15 kwenye Baraza la Madiwani la Arusha wakati CCM kimebakiwa kuwa na viti 12 wakati TLP ina viti sita.
Pia Chadema kina nafasi ya kuongeza kiti zaidi kwani ina nafasi moja ya viti maalum iliyokuwa ikishikiliwa na Rehema Mohamed aliyetimuliwa mwaka 2011.
Mwenyekiti wa madiwani wa Chadema, Isaya Doita alisema jana kwamba ushindi wa juzi ni chachu katika msimamo wa chama chao kutaka uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha urudiwe akiamini kuwa alichaguliwa kimizengwe.
Doita ambaye ni Diwani wa Ngarenaro, alisema wana imani muda si mrefu Jiji la Arusha sasa litapata Meya ambaye amechaguliwa kwa misingi ya sheria.
Chadema ilitetea viti vya Kata za Themi, Kimandolu, Kaloleni na Elerai ilivyovipoteza baada ya kuwafukuza waliokuwa madiwani wake kwa kosa la kukiuka maagizo ya Kamati Kuu ya chama hicho kuhusu mwafaka wa umeya.
Ushindi huo unakihakikishia wingi wa wajumbe katika baraza hilo la madiwani hivyo kuwa na fursa kumwondoa madarakani Meya Lyimo. Doita aliahidi kuwa chama hicho kitakaa leo kutoa msimamo kuhusu suala hilo la umeya wa Arusha.
Akizungumzia suala hilo, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alisema Chadema kisahau suala la kuchagua meya mpya kwani uchaguzi wake ulishapita.
Chatanda, ambaye pia anaingia katika vikao vya Baraza la Madiwani la Arusha kutokana na kuwa Mbunge wa Viti Maalumu, alisema Chadema kinapaswa kufanya kazi na meya wa sasa.
“Unajua vikao hivi vinaongozwa kwa kanuni, kwa hiyo wingi wao si hoja ya kumvua meya au kulazimisha kupitisha mambo yao,” alisema
Mamia wafurika Manispaa
Wabunge wanne wa Chadema jana waliongoza mamia ya wafuasi wa chama hicho katika shamrashamra ya kuwasindikiza madiwani wanne kwenda kujitambulisha kwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha.
Hata hivyo, furaha yao ilizimwa na polisi baada ya kumuomba Mbunge Arusha Mjini, Godbless Lema kuwatawanya.
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment