Sunday, September 15, 2019

TCRA yatangaza kuja kwa Kisimbusi kimoja kwa Chaneli zote nchini

0
tv chaneli decorder

Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA wametangaza kuja na kisimbusi kimoja kitakachoonyesha chaneli nyingi zaidi badala ya kuwa na kisimbusi (decorder) zaidi ya kimoja kuzipata zote.

Kisimbusi hicho kitakuwa na teknolojia ya cccam (card sharing) ambapo mtumiaji atakuwa anachomeka kadi maalum kupata chaneli anazokusudia badala ya kuwa na kisimbusi kingine.
kisumbusi kimoja
Kwa sasa ili kuweza kupata huduma za kitofauti basi inawalazimu watumiaji kumiliki visumbusi mbalimbali
Ni kwamba Kisimbusi hicho kitakuwa na uwezo wa kuingiza kadi maalumu itakayokupa fursa ya kupata Chaneli za aidha Azam, DSTV, Zuku, StarTimes, Digitek, Ting au Continental.
Mfano wake ni mtu kuwa na simu moja ambayo anaweza kuweka laini tofauti za kampuni za mawasiliano kupata huduma zao. Yaani kitakachokuwa kinabadilishwa ni cccam (card sharing) na sio Kisimbusi kama ilivyo sasa.
Mamlaka hiyo ya mawasiliano TCRA imeieleza kamati ya maendeleo ya kudumu ya Bunge kuja na mpango huo wa kuleta kisimbusi cha kuondoa kadhia ya kumiliki zaidi ya kisimbuzi kimoja.
kingamuzi kisambuzi tanzania tcra
Lengo kubwa linaonekana kurahisisha upatikanaji wa chaneli za bure. Utaratibu wa sasa umeathiri sana upatikanaji wa chaneli mbalimbali za kitanzania kwa baadhi ya huduma
Andrew Kisaka, mkuu wa kitengo cha leseni, amesema kwa kushirikiana na wadau wameweka utaratibu wa kuanza kuagiza Visimbuzi vya namna hiyo. Aidha amesema mtu yeyote anaweza kuagiza ila afuate utaratibu utakaowekwa.

Hata hivyo haijawekwa wazi itakuwaje kushare cccam (card sharing) kwa Chaneli ambazo zina tumia muelekeo wa setelaiti tofauti, je mtumiaji atalazimika kutumia zaidi ya Dishi moja au atalazimika kuligeuza kupata muelekeo wa Chaneli husika au TCRA yenyewe itakuwa na cccam server.

Mpango huo utaanza rasmi Desemba 31 mwaka huu.

Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment