Friday, August 30, 2013

KAPOMBE AFANYIWA UPASUAJI UFARANSA

0




BEKI kiraka wa AS Cannes ya Ufaransa, Shomari Kapombe hatarejea nchini kuichezea timu ya taifa, Taifa Stars kutokana na kufanyiwa upasuaji wa kidole cha mguu.
Kutokana na tatizo hilo, Kapombe atakuwa nje ya uwanja kwa siku 15 na tayari Kocha Mkuu Kim Poulsen, ametangaza kumuondoa katika kikosi chake.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Poulsen amesema kutokana na majeraha hayo, amemuondoa kiraka huyo kwenye kikosi chake kitakachoivaa Gambia, Septemba 8, ikiwa ni mechi ya kukamilisha ratiba ya kufuzu Kombe la Dunia 2014.
 “Nimemuondoa Kapombe kwenye kikosi changu kitakachoivaa Gambia kutokana na kuuguza kidonda alichofanyiwa upasuaji mguuni mwake.
“Kwa mujibu wa taarifa nilizopewa kutoka huko (Ufaransa), Kapombe anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa wiki mbili sawa na siku 15 akiuguza majeraha hayo kabla ya kuanza mazoezi mepesi.
“Alifanyiwa oparesheni hiyo kutokana na wadudu kuathiri sehemu ya kidonda alichopata akiwa huko, kidonda hicho kimesababisha ashindwe kucheza baadhi ya mechi akiwa huko,” alisema Kim.
Kapombe amejiunga na AS Cannes baada ya Poulsen kumruhusu aende kufanya majaribio ingawa Taifa Stars ilikuwa kambini kujiandaa kucheza na Uganda katika michuano ya Kombe la Chan.
Hata hivyo, kocha huyo hajaeleza kama ameshamuongeza beki mwingine kuchukua nafasi yake.
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment