Sunday, May 17, 2015

Lulu: Nyumba Niliyomzawadia Mama Sikuhongwa, Nimejenga Mwenyewe

0
Lulu: Nyumba Niliyomzawadia Mama Sikuhongwa, Nimejenga MwenyeweStaa mrembo wa Bongo Movies, Elizabeth Michel  ‘Lulu’amesema kuwa nyumba aliyomzawadia mama yake siyo ya kuhongwa bali amejenga mwenywe.
Lulu alieleza hayo kwenye mahojiano aliyoyafanya  na kipindi cha televisheni  cha The Sporah Show.
Je lulu aliwezaje kujenga nyumba hiyo ya kisasa?  Kwa kipato gani hasa anachokipata? Maswali haya yalilipelekea baadhi ya watu kudah labda alihongwa.
Lulu amelifungukia swala hilo kama ifuatavyo;
 “Kiukweli ile nyumba nimeanza kujenga nikiwa bado mdogo sana, ni nyumba ya chini ya kawaida lakini nilikuwa najenga kidogo kidogo, kwamba leo nikipata laki nampa mama leo kaongezee hiki…kwahiyo ni kwasababu mtu hajui atashangaa Lulu kapata wapi hela za vuuup, lakini ni kitu ambacho kimeenda kidogo kidogo imechukua hata miaka minne..kwahiyo mtu atashtuka kwasababu ameiskia leo sasa ndo hivyo mtu ataanza kusema kahongwa hajui background.” alisema Lulu.
Lulu alimzawadia mama yake nyumba  mwaka jana kwenye sherehe ya kuzaliwa ya mama yake kutimiza miaka 45 ya kuzaliwa.
Author Image

About tzfleva
Soratemplates is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design

No comments:

Post a Comment