Hit maker wa single mpya ya Nishike mkono D knob leo ame-amplify
sababu za kuamua kufunga ndoa ya kimya kimya mwaka 2009 huku idadi ya
watu waliohudhuria pamoja na maharusi wenyewe ikiwa sio zaidi ya 10
kuanzia kanisani mpaka walikoelekea baada ya kutoka kanisani.
Ameongea na millardayo.com na
kusema ‘nilitaka kuifanya na mwenzangu nikamwambia tumekua wapenzi
lakini sasa yahitaji tuwe ndani ya ndoa akasema twenzetu tukaongozana
mpaka kanisani padri akasema hamuwezi kuoana nyie mnajua hata ndoa ni
nini?kuna hatua’‘Siyo kitu ambacho tulitaka kufanya kama watu wengi wanavyofanya ile
kukaa kuchangishana kwa sababu mimi rafiki zangu wa karibu wote walikua
block nisingetaka kufunga ndoa halafu mwisho wa siku tuanze kununiana
kuwa huyu hajachanga yule kachanga chapili nilitaka kufanya ili
niendelee na maisha yangu kama mtu unapoamua kufanya birthday’
‘Wazazi walipata taarifa mwishoni kwa sababu hata mzee katika risala
yake maana tulikaa kwenye meza moja baada ya ndoa mzee akasema mimi
sijui nakupa zawadi gani maana umeniambia jana tu,kitu tulichofanikiwa
ni gauni la mke wangu maana ni gauni la gharama nashukuru Mungu lilitupa
stress mwanzo lakini liliwahi’.